SERIKALI wilaya ya Rorya mkoani Mara imewapongeza watafiti kutoka
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni ya jijini Dar es Salaam na Tume ya
Taifa ya Sayansi na teknolojia kwa kufanya utafiti katika wilaya hiyo na
kupeleka mbegu kinzani za mihogo katika wilaya hiyo.
Mkuu wa
wilaya ya Rorya Mkoani Mara Bw Elias Goloi ametoa pongezi hizo juzi kwa
watafiti waliofika wilayani humo kupeleka Mbegu kinzani za Mihogo
kufuatia utafiti uliofanywa na watafiti hao mwezi February Mwaka huu na kubaini
kuoza kwa mbegu za mihogo zilizokuwepo hapo awali.
Amesema
kupelekwa kwa Mbengu hizo kutasaidia kuondoa tatizo la kuoza kwa mbegu za
Mihogo wilayani humo na kusababisha tatizo la njaa wilayani humo,huku Mkuu wa
taasisi ya Utafiti Dr Joseph Ndunguru akisema kuandaliwa kwa Shamba la mfano
wilayani humo kutaleta tija kwa wakulima wa wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment