SERIKALI
imesema kuwa itahakikisha idara ya utafiti inabaki kuwa ni ya Muungano.
Waziri wa
sayansi , Teknolojia na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amebainisha hayo
mapema leo wakati akiongea na waandishi
wa habari kwenye maonesho ya Muungano yanayoendelea kwenye viwanja vya mnazi mmoja
jijini Dar es salaam.
Profesa
Mbarawa amefafanua kuwa wizara ya sayansi na teknolojia ina jukumu la kusimamia
na kusambaza ubunifu na teknolojia mbalimbali bara na visiwani ili kuboresha maisha ya
mtanzania .
Amesema
vitu muhimu kwenye mawsiliano ni masafa , ambayo kwa sasa Tanzania bara na
visiwani ina namba moja ya masafa iliyopewa na shirika la mawasiliano Duniani (ITU
)yenye makao yake makuu Geneva, Uswisi hivyo kama itatokea kuvunja Muungano itabidi kila nchi iwe na masafa
yake.
No comments:
Post a Comment