WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda amewanasihi watanzania kutumia
dfursa zilizopo za muungano ili kujiimarisha kiuchumi na kijamii.
Mheshimiwa
Pinda ameyasema hayo leo katika viwanja vya Mnazi momoja wakati akifunga
maonesho ya Muungano yaliyoanza siku ya jumatano wiki hii.
Amesema
kuwa, ni kweli Muungano unachangamoto zake lakini serikali inachukua hatua
mbalimbali katika kukabiliana na changamoto hizo.
Amesema
fursa zilizopo ni pamoja upande wa Bara kuwa na idadi ya watu wengi ikiwa na
watu milioni arobaini na mbil huku Zanzibar ikiwa na watu milioni moja na laki
tatu , hivyo ni muhimu kuzitumia fursa hiziza uwiano wa idadi ya watu katika
kupanua wigo wa shughuli za kiuchumi na kijamii katika nchi hizi mbili
No comments:
Post a Comment