ZAIDI ya wahamiaji haramu 30 kutoka nchini Burundi
wamekamatwa na idara ya uhamiaji mkoani Kagera
baada ya kutoroka kwenye kambi ya wakimbizi iliyoko nchini Uganda na kuingia hapa
nchini kinyume cha sheria.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari hapo jana Afisa uhamiji mkoa wa Kagera George
Kombe, amesema kuwa wahamiaji hao haramu 30 walikuwa wakihifadhiwa katika
kambi ya wakimbizi ya Nakivale iliyoko nchini Uganda, lakini walitoroka
na kuingia nchini Tanzania kupitia mpaka wa Bugango ulioko
wilayani Misenyi, na kukamatwa baada ya wananchi kutoa taarifa katika ofisi za
uhamiaji.
.
Wakiongea
katika mahojiano na Maafisa wa idara ya uhamiaji, baadhi ya wakimbizi hao
walipoulizwa kuhusiana na tatizo lililowafanya watoroke katika Kambi hiyo,
wamedai kukimbia huduma duni ikiwemo kutopewa huduma muhimu hasa chakula,
hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha yao, na kuomba kama kuna uwezekano wa
kwenda kambi ya Nyarugusu haupo ,basi wapelekwe kwao Burundi.
No comments:
Post a Comment