Saturday, April 19, 2014

WAWEKEZAJI watakiwa kuyaendeleza maeneo ya ardhi



WIZARA   ya  ardhi nyumba na maendeleo ya makazi  imesema hakuna sababu ya wawekezaji kuhodhi  maeneo  makubwa ya ardhi  pasipo kuyaendeleza  huku wananchi wakiendelelea kuteseka  ambapo serikali    inakusudia   kuchukua  hatua  za  kuwanyang’anya   maeneo  hayo na   kuyagawa   kwa wananchi wasio na ardhi  ili yaendelezwe kwa shughuli za kilimo  .

Naibu waziri  wa  Ardhi,  nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa          George Simbachawene ameyaeleza hayo hivi karibuni mkoani  Morogoro wakati akizungumza na mtandoa wa vikundi vya wakulima wadogo nchini MVIWATA,ambapo amesema  halmashauri nchini zinatakiwa kufanya kazi  kwa uadilifu kusimamia sheria na mpango wa matumizi bora ya ardhi  na kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya kumiliki ardhi.

Nae  Mkurugenzi wa mtandao  wa  vikundi vidogo vya wakulima (MVIWATA) Bwana Ste  Ruvuga amesema  wakulima wangependa kuona katiba mpya inatoa  ulinzi na haki katika kumiliki ardhi ili kupunguza  migogoro ya ardhi katika mikoa mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment