BODI ya maji katika mji wa
Branytre nchini Malawi umeanzisha huduma
ya ujumbe mfupi kwa njia ya simu ya kiganjani ili kurahisha upatikanaji wa
taarifa mbalimbali kwa wateja wake.
Afisa wa bodi anayeshughulikia masuala ya umma Bi Priscilla Mateyu
ameeleza hay oleo kupitia taarifa yake kwa umma na vyombo vya habari nchini
humo, kuwa kupitia taarifa hiyo mteja wa maji atapata kufahamu ankra za malipo
ya uzilizopita na za sasa , taarifa za kukatika kwa maji na huduma za maji
zinazotolewa na bodi hiyo.
Bi mateyu amesema kuwa .utafiti umebaini kuwa, wananchi wengi
nchini humo hawana uwezo wa kupata taarifa kupitia redio, runinga na hata
magazeti, hivyo huduma hiyo itaondokea kero kwa wateja wao.
No comments:
Post a Comment