WAZAZI na walezi nchini wameonywa kutowageuza
wanafunzi kuwa “yaya’ wa kuwalea watoto ili kupunguza kasi ya wanafunzi
wasiojua kusoma , kuandika na kuhesabu .
Rai hiyo imetolewa na wadau wa elimu wilaya ya Katavi, mkoani
Katavi katika mahojiano maalum wakati wakati wakitahmini hali ya elimu wilayani
humo.
Wameeleza kuwa, tafiti za elimu zimebaini kuwa , wanafunzi
wengi hawahudhurii darasani kutokana na kupangiwa majukumu ya kulea wadogo zao
nyumbani na hivyo ku uwanyuma kitaaluma.
Wilaya ya Katavi mkoani Katavi ina jumla ya wanafunzi 1500
wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu (kkk), ambapo tafiti hizo zimebaini kuwa
wilaya ya Mwanga ,mkoani Kilimanjaro ina wanafunzi 1655 wasiojua kusoma ,
kuandika na kuhesabu kwa kipindi cha mwaka 2013/2014, wanafunzi hao ni wa kuanzia
darasa la tatu hadi la saba.
No comments:
Post a Comment