Tuesday, May 13, 2014

WIZARA ya kilimo yaandaa muswada wa sheria kuanzisha mfuko wa kuwasaidia wakulima



MFUMO wa masoko ya mazao ya kilimo unakabiliwa na kukosekana kwa  taarifa sahihi na miundo mbinu mibovu.

Waziri wa kilimo, chakula na ushirika Mheshimiwa Christopher Chiza ameeleza mwmwhishoni mwa wiki mjini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya wizara ya yake kwa matumizi ya mwaka 2014/2015

Amesema, kutokana na hali hiyo wizara kwa kushirikiana na wakala wa mazao husika inaandaa utaratibu wa kuanzisha mfuko wa mazao kwaajili ya kusaidia wakulima pindi bei ya mazao inaposhuka katika soko la dunia.
Muswada wa sheria ya kuanzisha mfuko wa kufidia bei ya mazao unatarajiwa kuwasilishwa bungeni katika kipindi cha mwaka 2014/2015


No comments:

Post a Comment