Saturday, May 10, 2014

MANISPAA ya Morogoro yawawezesha vijana wafanya biashara ya mbao



.
MEYA wa Manispaa ya Morogoro mheshimiwa  Amir  Nondo amesema kuwa uongozi wa Manispaa hiyo  umefanikiwa  kuwapatia mikopo  vijana zaidi ya 200 wa  kongano mbalimbali ili waendeleze mitaji yao.

Mheshimiwa Nondo ametoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza katika uzinduzi  wa kongano la wafanya biashara wa mbao waliopo ndani ya manispaa hiyo.

Pamoja na kuzungumzia suala la  mikopo  pia amesema kuwa Halmashauri  ya manispaa ya Morogoro inakusudia kutafuta  eneo la kupanda miti  kwa ajili ya vijana   zaidi ya 70 wa kongano la mbao lengo likiwa ni kupunguza ukataji  wa miti na kuzuia  uharibifu wa mazingira.

No comments:

Post a Comment