Saturday, May 10, 2014

KAMPUNI ya African Barrick yalipa Halmashauri ya Tarime shilingi bilioni 1 kama tozo ya huduma


KAMPUNI ya uchimbaji Madini ya African Barrick inayomiliki Mgodi wa North Mara imelipa kiasi cha Dola laki nane sawa na shilingi Bilioni 1 na milioni mia 300 kwa halmashauri ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara ikiwa ni tozo ya huduma kwa kipindi cha Mwaka 2002 hadi 2005.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika baraza la Madiwani la halmashauri ya wilaya ya Tarime mkoani Mara mbele ya Naibu waziri wa nishati na Madini mheshimiwa Steven Masele.

Bw Masele amesema kuwa pamoja na kukamilika kwa Malipo hayo  mgodi huo unatakiwa kukamilisha yale yote ambayo wamekubaliana ikiwa ni njia ya kuondoa malumbano ya mara kwa mara kati ya Mgodi na viongozi wa halmashauri hiyo.
 .
Kwa Mujibu wa Naibu waziri  Masele  mpaka sasa halmashauri nne hapa nchini zimelipwa Tozo ya huduma ambayo ni Shilingi Bilioni 8 kutoka katika Makampuni ya Migodi iliyopo katika halmashauri hizo huku viongozi wa halmashauri ya Tarime wakiahidi kuelekeza fedha hizo katika Miradi ya Maendeleo. 

No comments:

Post a Comment