Friday, May 9, 2014

RAISI Kikwete amteua Rished Bade kuwa kamishina mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania



RAISI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni  Sefue, uteulzi huo umaanza tangu  Mei sita mwaka huu ambapo Bwana BADE anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu  Desemba 14,mwaka jana.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangu Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangia Bwana Kitilya alipostaafu.
Kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi kufanya kazi katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa kwenye mambo ya fedha na mapato.
 Mheshimiwa Rais ana imani kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished Bade kwa kushirikiana na watumishi wenzake, katika kutoa mchango  kwa Taifa na kuzidi kuimarisha Mamlaka hiyo na kuboresha utendaji wake na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa faida ya Taifa.


No comments:

Post a Comment