MJUMBE Maalum wa Umoja wa Mataifa
kuhusu Elimu ya Kimataifa na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza,bwana
Gordon Brown amesema kuwa Tanzania imefanya vizuri zaidi kuliko nchi nyingine
yoyote ya Afrika katika uandikishaji wa watoto kuanza shule.
Bwana Brown amekutana na Rais Kikwete kwenye
Hoteli ya Hilton mjini Abuja ambako wote wawili wanakaa kwa ajili ya kuhudhuria
Kongamano la Uchumi Duniani – kwa Bara la Afrika lilioanza jana katika mji mkuu
wa Nigeria Abuja.
Kwa sababu hiyo na kwa
sababu ya mafaniko hayo Brown amesema kuwa Umoja wa Mataifa na Taasisi zake na nyingine za kimataifa ziko tayari kuisaidia
Tanzania kufikia lengo la kusajili watoto wote kwa asilimia 100 ya watoto
wanaotakiwa kuingia shule katika muda wa uongozi wa Rais Kikwete na kabla
hajaondoka madarakani mwishoni mwa mwaka ujao.
.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu,Rais Kikwete pia amekutana
na kufanya mazungumzo na Bwana Mark Suzman, Mkurugenzi wa Sera na Mipango
wa Taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani. Aidha, Rais amekutana na
kufanya mazunguzo na Bwana Sunnil Bharti Mittal, Mwenyekiti wa Kampuni ya
kimataifa ya simu ya Airtel duniani.
No comments:
Post a Comment