JAMII na serikali imetakiwa
kutoa ushirikiano kwa wakunga kwa lengo la kuhakikisha kuwa mama wajawazito
wanapata huduma stahiki toka kwa wataalamu hao wa afya ili kupunguza vifo vya
mama na mtoto.
Nasaha hizo zimetolewa hivi karibuni na Raisi wa
chama cha wakunga nchini Dk Fredy mwanga katika maadhimisho ya siku ya wakunga
duniani yaliyofanyika mnazi mmoja jijini
Dar es salaam.
Dk Mwanga Amesema kuwa, kuna baadhi ya wakunga wanakiuka
maadili ya kazi kwa kutoa lugha chafu kwa kina mama wajawazito wanapotoa huduma
hali inayopelekea wananchi kuwachukia baadhi yao na kuilahumu serikali ilihali
ukunga ni taaluma inayoongozwa kwa maadili ya kazi kama zilivyotaaluma nyingine.
Kutokana na hali jamii imeombwa kutoa taarifa kwa
waganga wakuu wa hospitali za wilaya na mkoa sanjari na vituo vya afya endepo
patatokea udhalilishaji toka kwa wakunga ili sheria ichukue mkondo wake..
No comments:
Post a Comment