Tuesday, May 6, 2014

UJANGILI wachangia kushuka kwa watalii nchini

KUSHAMILI  kwa ujangili katika hifadhi za Taifa zilizopo hapa nchini  kunasababisha kupungua kwa watalii  kuingia kwa wingi  kutokana na baadhi ya wanyama pori kutoweka na kuziacha hifadhi hizo kutokuwa na wanyama wa kuvutia.

Akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Umoja wa wanafunzi wanaosomea mambo ya wanyamapori katika Chuo Kikuu cha  Kilimo Cha Sokoine,Afisa masoko kutoka  Bodi ya Utalii nchini Bwana Peter Mkumbo  amesema  sababu kubwa ya kupungua kwa watalii hapa nchini inatokana na kuongezeka kwa ujangili katika hifadhi hizo.

Aidha Bwana Mkumbo amefafanua kuwa kupungua kwa hoteli za kulala watalii pia ni sababu moja wapo ya kupungua kwa watalii nchini ambapo kwa sasa wanamikakati ya kuhamasisha wawekazaji kuwekeza katika maeneo hayo ili  kulisaidia Taifa kuongeza watalii na kuongeza kipato.

No comments:

Post a Comment