Wednesday, May 7, 2014

VYAMA vya msingi vya ushirika mkoani Kilimanjaro vitaanza kujiendesha vyenyewe katika kukusanya kahawa



VYAMA vya msingi vya ushirika wa wakulima wa kahawa mkoani Kilimanjaro vitaanza kujiendesha vyenyewe katika shughuli za kukusanya kahawa kutoka kwa wakulima na kuipeleka sokoni kuanzia  msimu huu wa 2014 badala ya chama kikuu cha msingi cha ushirika cha KNCU.  

 Meneja mkuu wa KNCU Bw Honest Temba amesema maamuzi hayo yamepitishwa na mkutano mkuu wa chama hicho ,uliyofanyika hivi karibuni kwa lengo la kuviwezesha vyama hivyo ,kuendesha shughuli zao kwa ufanisi zaidi.

Bw. Temba amesema mkutano mkuu umependekeza kuwa ,ili wakulima na vyama hivyo viweze kunufaika na kilimo cha kahawa ,KNCU itavijengea uwezo vyama hivyo kwa kuvipatia elimu ya kujiendesha ,hususani katika biashara ya kahawa pamoja na kusimamia fedha zao wenyewe  sambamba kukabiliana na changamoto mbalimbali.

No comments:

Post a Comment