WAKULIMA wa zao la mahindi na alizeti wialayni Mpwapwa mkoa wa Dodoma wameiomba serikali kuwapatia elimu ya kilimo bora na cha kisasa ili kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuzalisha mazao ya chakula na biashara.
Wakiongea na mbiu ya maendeleo mjini Mpwapwa jana , wakulima hao wa kijiji cha Pwaga wameeleza kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yanatokea kwa kasi kubwa sana hapa nchini hivyo wataalamu wa kilimo wanachangamoto kubwa ya kuwapatia wakulima mbinu zitakazowawezesha kukabiliana na hali hiyo ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
No comments:
Post a Comment