WAZIRI MKUU Mheshimiwa
Mizengo Pinda amesema shule za msingi hapa nchini zinakabiliwa na upungufu wa
madawati yapatayo milioni moja na nusu ambapo ameitaka Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi ijifunge mkanda na kulipa kipaumbele suala la kupunguza
tatizo hilo.
Waziri Pinda metoa agizo hilo jana wakati akiwahutubia
mamia ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma ambao walihudhuria
uzinduzi wa Wiki ya Elimu Tanzania kwenye uwanja wa Jamhuri.
Kutokana na mahitaji hayo, Waziri Mkuu amesema
endapo Serikali itaamua kutengeneza madawati 100,000 kwa mwaka kwa gharama ya
sh. bilioni 12/ itachukua miaka 15 kumaliza tatizo hilo ili kuziba pengo lililopo
sasa.
Mheshimiwa Pinda amesema ni lazima hatua madhubuti
zichukuliwe kumaliza tatizo hilo kwani inatia aibu na hakuna sababu ya
kuendelea kuona wanafunzi wakisoma huku wamekaa chini.
Wakati huohuo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Dodoma, Profesa Idris Kikula, akitoa shukrani kwa niaba ya wadau wa elimu
alisema anaunga mkono hoja ya uchangiaji wa madawati na kusisitiza kuwa kuna
haja ya watu kubadili mtazamo walionao kuhusu suala la uchangiaji wa huduma za
kijamii.
No comments:
Post a Comment