SHIRIKA la kuhifadhi misitu ya
asili Tanzania (TFCG) kupitia mradi wa kuongeza thamani katika
misitu AVA limeanza kuhamasisha jamii zinazoishi kando kando ya misitu kujiunga
katika vikundi vya hisa ili kupunguza uharibifu wa mazingira.
Hayo yameelezwa na Meneja wa Mradi wa AVA Bwana Hassan Chikira na
kusisitiza kuwa mradi huo unatekelezwa katika vijiji 31 vilivyomo katika
wilaya ya MVOMERO mkoani Morogoro.
Bwana Chikira amesema uanzishwaji wa vikundi hivyo kupitia mradi
wa AVA utawarahisishia wananchi wanaoishi kando ya misitu kupata fedha za
kuendesha miradi mingine na kuacha kutegemea misitu kama chanzo cha mapato yao.
.
Mradi wa AVA umelenga kuhakikisha jamii inayozunguka misitu
inaacha tabia ya kutumia misitu kama chanzo cha kipato ili waweze
kuhifadhi mazingira.
No comments:
Post a Comment