Saturday, May 3, 2014

UMOJA wa wanawake wa chama cha mapinduzi mkoani Mara wakemea na kulaani matukio ya mauaji ya wanawake



UMOJA wa wanawake  wa Chama Cha Mapinduzi  (UWT) mkoani Mara, Umekemea vikali na kulaani matukio ya mauaji dhidi ya wanawake yanayoendelea katika maeneo mbalimbali katika mkoa huo.

Tamko la kulaani mauaji hayo limesomwa jana na katibu mkuu wa UWT mkoa wa Mara Bi. Hellena Chacha katika ukumbi wa CCM mkoani Mara kwa niaba ya mwenyekiti wa umoja huo Bi. Nancy Msafiri.

Amesema mauaji hayo ya kikatili yasiyo na kikomo kwa wilaya ya Butiama yanalaaniwa kwa nguvu na UWT mkoani Mara na kuiomba serikali kuchukua hatua katika kukomesha mauaji hayo na kuifanya Butiama kuwa kanda Maalum ya kipolisi.
 .
 Mauaji ya wanawake katika mkoa wa Mara yamekuwa yakitokea mara kwa mara na hivyo kutishia uwepo wa tatizo la njaa kutokana na wanawake hao kushindwa kwenda shambani ambako ndiko wauaji hutekeleza azma zao hizo ikihusishwa na vitendo vya kishirikina.

No comments:

Post a Comment