MKAKATI maalum wa kuwasaka
magaidi na majambazi nchini Kenya umekamata zaidi ya watu 1500 wanaoishi
kinyume cha sheria nchini humo.
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Kenya IGP David Kimaiyo ameeleza
hayo mapema jana wakati akiongea na vyombo vya habari kuutaarifu ulimwengu hali
halisi ya msako huo ambao ni endelevu mpaka
hapo hali itakapokuwa shwari.
Kamanda Kimaiyo amesema
watu hao 1500 waaliokamatwa katika
opresheni wanatoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania, Somali, Uganda,
Burundi na Sudani.
Ameafafanua kuwa waliorejeshwa ni wale ambao hawana vibali vya
kisheria vya kuishi nchini Kenya na hakuna ubaguzi katika operesheni hiyo.
No comments:
Post a Comment