Sunday, May 4, 2014

VIONGOZI wametakiwa kuwa waaadilifu ili kuwaletea maendeleo wananchi



VIONGOZI  wametakiwa  kuwajibika  na kuwa waadilifu ili kuhakikisha kuwa wanawaletea maendeleo wananchi kkatika muda muafaka.

Mbunge wa jimbo la Ubungo Mheshimiwa John Mnyika ametoa rai hiyo mapema jana katika kikao cha kujadili ujenzi wa Zahanati ya  mtaa wa Malamba mawili kata ya Msigani jimbo la Ubungo,jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Mnyika amefafanua kuwa ni jambo la busara kwa wananchi kushirikiana na viongozi kiujiletea maendeleo huku wakisubiri serikali kutekeleza ahadi iliyo waahidi wananchi wake.
Katika kikao hicho Mheshimiwa Mnyika alichangia shilingi milioni kumi kwaaajili ya ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa Malamba mawili kata ya Msigani ,Manispaa ya Kinondoni , jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment