Saturday, May 17, 2014

WAHUBIRI wa dini ya kiislamu wahimizwa kuhubiri mshikamano na kuepuka mahubiri ya uchochezi



WAHUBIRI na wahadhiri wa Dini ya kiiislam nchini wametakiwa kujikita katika kuhubiri Umoja na mshikamano katika jamii na sio kuhubiri ubaguzi,uchochezi au kuletea mgawanyiko ambao unaweza kujenga chuki miongoni mwa jamii na kusababisha taifa katika migogoro na Vurugu.

Wito huo Umetolewa na Naibu Mufti wa baraza kuu la waislam Tanzania(BAKWATA)Sheikh Ali Muhiddini Mkoyogole wakati akifungua semina ya siku mbili ya wahadhiri na wahubiri wa dini ya kiislam kutoka mikoa mbali mbali nchini iliyoandaliwa na Taasisi ya kiislam ya Charity People Trust ambayo inajishughulisha na utoaji huduma kwa jamii.

Amesema Machafuko katika nchi mbali mbali yanatokana na maeno ya Uchochezi au mahubiri yanayopandikiza chuki katika misingi ya dini,itikadi na baadae nchi hizo hujikuta katika migogoro ya muda mrefu na hatimaye husababisha vita .

Kwa upande wake Rais wa Taasisi hiyo Sheikh Abdallah Ndauka amesema madhumuni ya kuandaa semina hiyo yanatokana na kuwepo kwa mgawanyiko na mahubiri yanayokwenda kinyume na uislam ambayo yanaweza kupandikiza chuki katika jamii.

1 comment:

  1. ujumbe muhimu sana hasa kwa wakati tulio nao,,, matatizo ya waislamu yana majawabu yake sio fujo,, pia kuna methodology yake ,,

    ReplyDelete