AFISA Mtendaji wa kijiji cha Kivukoni Wilayani Ulanga,mkoani
Morogoro Seth Maunga,amemburuza makamani Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU na Kamanda wa Taasisi hiyo Wilayani Ulanga akidai kulipwa fidia ya shingi Mil.150 kwa kumdhalilisha na kumnyanyasa akiwa kazini
Katika kesi hiyo ya jinai namba 86/2014 I aliyoifungua na kusajiliwa 20/Mei Mahakama kuu ya Dar es salaam,Maunga aliyekuwa Mtendaji wa kijiji cha Milola wakatia akitendewa hayo alisema uamuzi huo unatokana na kubaini kuwa taasisi hiyo haikumtendea
haki kwa mujibu wa sheri baada ya kumchunguza kwa zaidi ya Miaka mitatu badala
ya miezi sita.
Kwa mujibu wa Maunga Taasisi hiyo wakati
ikimchunguza ilikuwa ikieneza taarifa za kumchafua na kuzuia utendaji wake kwa
kukusanya nyaraka muhimu na vitendeakazi vya ofisi yake na kukaa navyo kwa muda
mrefu jambo lililomwongezea ugumu katika utumishi wake huku akionekana mwizi kutokana na
harakati ambazo amekuwa akifanyiwa waziwazi.
Akizungumzia udhalilishaji na unyanyasaji huo,Maunga alisema katika uchunguzi wake ulioanza Desemba 2009 hadi 24/3/2010 Takukuru Ulanga walimfanyia uchunguzi na kuchukua bila ridhaa yake nyaraka za serikali kinyume na sheria ya Takukuru namba 11 ya 2007 kifungu cha 9(1)(2)na(3) .
“kwa mujibu wa sheria hii nilipaswa kufikishwa mahakamani lakini kwa makusudi hawakufanya hivyo kwa zaidi ya miaka mitatu kunidhalilisa,
hata hizi gharama nilizoainisha hapa zitaongezeka kutokana na mwenendo wa kesi sambamba na ongezeko la gharama hadi hapo kesi itakapokwisha”aliongeza.
Mwandishi wa habari hizi alipomtafuta kamanda wa Takukuru wilayani humo Innocent Shetui kutoa ufafanuzi hakutaka kuonyesha ushirikiano wa kutoa ufafanuzi huo huku akiwataka waandishi hao kuwasiliana na mkurugezi wa Takukuru nchini Edward Hosea.
No comments:
Post a Comment