Friday, June 6, 2014

MKUU wa mkoa awaagiza wakurugenzi wa wilaya kuwaripoti watumishi wa serikali wazembe na wasio waadilifu ili wachukuliwe hatuataarifa


MKUU wa mkoa wa Morogoro DK Joel Bendera amewaagiza wakurugenzi wa wilaya mkoani Morogoro kupeleka haraka taarifa ya watumishi wa serikali  wazembe na wasio waadilifu ofisini kwake ili awachukulie hatua za kisheria.

Bendera ametoa agizo hilo mjini Morogoro  katika kikao cha madiwani halmashauri ya morogoro cha  kupitia majibu ya hoja za mkaguzi mkuu wa waserikali (GAG)mwaka 2012\ 2013
.

Dk Bendera alisema hayo baada ya kusoma taarifa ya CAG ambayo imeonesha mkoa huo kufanya vizuri katika hesabu zakehususani  katika ofisi ya mkuu wa mkoa na mamlaka za serikali za mitaa na kupata hati safi isiyona mashaka 2012na 2013.

Pamoja na mkoa  kupata hati safi ktika hesabu za mwaka 2012 na 2013 Bendera amewataka watumishi wake kutoridhika na mafanikio hayo na baadala yake waendelee kupambana ili kuweza kupambana ili kudumisha mafanikio kwa lengo la kufikia kiwango cha juu kabisa.

Mbali na hilo amezipongeza halmashauri hususani ya wilaya ya Morogoro kwa kukataa kupata hati chafu kama ilivyokuwa mwaka 2010 na 2011.
















No comments:

Post a Comment