TAFITI zinaonesha
kuwa asilimia 90% ya watanzania wanategemea nishati ya mkaa katika matumizi
mbalimbali hasa waishio vijijini ambao hutegemea uchomaji wa
mkaa kuwa chanzo cha kujipatia kipato.
Wakiongea na Mbiu ya Maendeleo hivi karibuni katika kijiji cha Msimba wilayani Kilosa,mkoani Morogoro
,wafanyabiashara ya mkaa wamesema kuwa hali hiyo imejitokeza katika maeneo
mengi hapa nchini baada ya wananchi wanaoishi kandokando ya misitu
kujishughulisha na uchomaji wa mkaa ikiwa ndio shughuli kuu ya kuwapatia
kipato.
Kupitia mradi wa mkaa endelevu uliopo chini ya shirika la
kuhifadhi misitu ya asili Tanzania TFCG unafadhiliwa na shirika la maendeleo la
USWISS wananchi wanaochoma mkaa wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wameiomba
serikali kusogeza karibu huduma ya upatikanaji wa vibali na leseni za ukataji
wa miti katika vijiji vyao ili kupunguza usumbufu wa ufuatiliaji vibali hivyo
katika ofisi za wilaya.
No comments:
Post a Comment