SERIKALI wilayani Kilosa imetaja miradi itakayo zinduliwa na mbio za mwenge mwaka huu ndani ya wilaya ya Kilosa.
Akizungumzia miradi hiyo juni 11 mwaka huu Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo mnamo june 23 mwaka huu mwenge utapokelewa ukitokea wilaya ya kilombero na kukimbizwa wilayani kilosa , Ukiwa ndani ya wilaya ya Kilosa mwenge huo utazindua miradi saba ambayo ni pamoja na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji mikumi uliyogharimu jumla ya shilingi milioni mia nane , kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa kukoboa ya vijana Ilakala, kuweka jiwe la msingi katika hosteli ya shule sekondari isanga , ufunguzi wa kituo cha kupima VVU ulaya .
Amesema
miradi hiyo ambayo imegharimu fedha nyingi ni lazima wananchi waakikishe
inaendelezwa na si kufia njiani kama inavyojitokeza katika baadhi ya miradi
inayoanzishwa , kwani hayuko tayari kuona miradi ikiteketea na kuona fedha za
wananchi zikipotea bila kuleta faida .
Mwenge
huo utakimbizwa ndani ya wilaya ya Kilosa kwa siku moja na utalala kata ya
kisanga kabla ya kukabidhiwa kwenye uongozi wa mkoa ambapo ndipo
utakapo kuwa mwisho wa mbio za mwenge katika wilaya ya Kilosa
mkoani Morogoro baada ya hapo uongozi wa mkoa utaukabidhi mwenge huo mkoani
Iringa .
Pia
ametoa wito kwa wananchi wa kilosa kutoa michango ili kufanikisha mbio hizo
kwani hadi kukamilisha mbio hizo zinahitajika milioni 30 na kusema kuwa
hadi sasa wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 15.
No comments:
Post a Comment