Wanafunzi wa shule ya msingi Chamwino Manispaa ya Morogoro wakicheza
WATANZANIA wataungana na Watu wengine Barani Afrika
kuadhimisha siku ya mtoto Afrika inayotarajiwa kuadhimishwa tarehe 16 mwezi
huu.
Akizungumza na Mbiu ya Maendeleo
mratibu wa maadhimisho hayo Grace Chagongwe amesema kwa wilaya ya Kilosa
yatafanyika kijiji cha Nyali tarafa ya Ulaya ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa Mkuu wa Wilaya Kilosa Elias Tarimo
.
Chagongwe amesema lengo la
maadhimisho hayo ni kuwakumbuka watoto waliuwawa kikatili kwenye
kitongoji cha SOWETO nchi Afrika Kusini kulihamasisha na kukumbusha jamii
juu ya haki wanazopaswa kuwapatia watoto na kupata taarifa mbalimbali
zinazohusu watoto.
Amesema kwa kiasi kikubwa watu
wanahamasika kufuata haki za watoto hasa swala la Elimu
Aidha ameyataja mafuriko
yaliyopatikana kutokana na maadhimisho hayo ni pamoja na kuandikishwa kwa
watoto wenye umri wa kwenda shule kwa asilimia 83.12 ufaulu wa wanafunzi
wanaomaliza elimu ya msingi kwa asilimia 60 na watoto waliokuwa mazingira hatarishi
ikiwa ni pamoja na yatima kulipiwa ada za shule.
Kauli mbiu ya mwaka huu katika
maadhimisho hayo ni KUPATA ELIMU BORA NA ISIYO NA VIKWAZO
No comments:
Post a Comment