MKAZI wa mjini kilosa,mkoa wa
Morogoro aliyetambulika kwa jina la Abdallah Ramadhani aliyekadiliwa kuwa na
umri wa miaka 60 ambaye alikuwa mlinzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi ( CCM)
wilayani Kilosa amekutwa amefariki usiku wakuamkia juni 12 mwaka huu
Akizungumzia kifo hicho mtoto wa
marehemu Ramadhani Abdallah amesema kuwa baba yake alikuwa anasumbuliwa na
ugonjwa wa shinikizo la damu na alipatiwa matibabu juni 9 mwaka huu na kuambiwa
arudi juni 12 kwa matibabu zaidi, na ameongeza kwa kusema kuwa marehemu baba
yake ameacha watoto tisa na wake watatu.
Akifafanua tukio hilo katibu wa
chama cha mapinduzi Wilayani Kilosa Dodo Sambu amesema kuwa mlinzi huyo ni
kweli alikuwa akifanya kazi katika ofisi hiyo ila hawakuwa na taarifa yoyote ya
ugonjwa ya mlinzi huyo.
Akithibitisha tikio la kifo hicho
hicho kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya kilosa masale Dickson
ameeleza chanzo cha kifo hicho kuwa ni tatizo la shindikizo la damu lililokuwa
juu sana na ndio lililompelekea kifo chake.
No comments:
Post a Comment