UZINDUZI wa kampeni ya kuchangia damu salama
umefanyika leo katika ukumbi wa Anatoglu manispaa ya Ilala ambapo watatnzania
wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuchangia damu kwaajili ya kuwapatia
wahitaji.
Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Anatoglu
jijini Dar es salaam mapema leo ,Afisa viwango na ubora wa damu salama kanda ya
mashariki ,Bwana Ndeonasi Towoa amesema kuwa watanzani wanatakiwa kujenga
utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mrasanjari na utoaji wa damu kwaajili ya kupunguza vifo kwa kinamama wajawazito na watu
wengine wenye mahitaji.
Kilele cha maadhimisho ya kampeni hiyo kinatarajiwa
kufanyika juni 22, kwenye viwanja cya
sitakishari, kata ya Kipawaa ,jijini Dar es salaam.
Kitaifa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu salamakwa kina
mama wajawazito ili kupunguza vifo inafanyika kesho mjini Tabora na mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa mke wa Raisi Salma Kikwete.
No comments:
Post a Comment