Wananchi wakiangalia mabaki ya soko la Mchikichini Ilala, Dar es salaam |
WAFANYABIASHARA wa soko la Mchikichini lililopo Manispaa
ya Ilala jijini Dar es salaam wameitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina
kubaini chanzo cha moto uliotoke usiku
wa kuamkia jana ili kubaini ukweli na kisha kuwa juza wafanyabishara na
wananchi kwa ujumla.
Wakiongea na Mbiu ya Maendeleo katika soko hilo leo ,
wafanyabiashara hao wameeleza kuwa wanashaka
na kilichotokea kwani kuna mazingira tatanishi hivyo uchunguzi wa kina
na taarifa iliyowazi itawafanya waondoe shaka waliyonayo.
Soko la mchikichini la Ilala, jijini Dar es salaam
liliunguza jana na kusababisha hasara kubwa za mali za wafanyabishara na
majengo ya serikali ambapo mpaka sasa hasara kamili ya mali zilizopotea
haijajulikana kwani uongozi wa manispaa na Ilala na mkoa umekuwa katika kikao
kujadili hali hiyo na kisha baade kutoa tathmini ya hali halisi ya hasara
No comments:
Post a Comment