Wednesday, June 11, 2014

SHIRIKA la HUDESA latoa mafunzo ya lishe kwa kinamama wilayani Kilosa



SHIRIKA  lisilo la kiserikali HUDESA hivi karibuni  limetoa mafunzo  ya lishe bora kwa mtoto  kwa vitendo kwa kina mama wa wilayani Kilosa mjini,mkoani Morogoro.


Naye  Mkaguzi wa shirika hilo la HUDESA Mkoa wa Morogoro Deus Ngerangera  amesema kuwa kufuatia mafunzo waliyopewa yataweza  kunusurru maisha ya watoto kwa kupewa lishe bora na kuwataka wananchi kulima viazi vitamu vya njano kwa ajili ya kupata vitamin “A” pamoja na mboga za majani piawamejifunza kuandaa lishe bora kwa mtoto na kuandaa chakula cha mtoto cha aina tatu ambapo ni uji wa mahindi , uji wa ulezi , pamoja na uji wa viazi.

Kwa upande wake mratibu wa mradi wilaya ya kilosa Antony  Fuime ameeleza kuwa wilaya ya kilosa ipo kwenye haIi mbaya katika lishe ya watoto kwa kusema kuwa ni wilaya ya mwisho ukilinganisha na wilaya nyingine katika mkoa wa morogoro.

Nao maafisa lishe wilaya ya Kilosa Zainabu  Waziri na Zaina Kibona wamewataka kina mama wa wilaya Kilosa kuzingatia lishe hiyo waliyojifunza kwani itawajengea uwezo mzuri watoto kiakili na kiafya na kuongeza kuwa wazazi wanatakiwa kujishughulisha kwa kilimo kwa ajili ya kuwapatia hamu ya kula.


No comments:

Post a Comment