Monday, June 30, 2014

BAN Ki moon kukutana na Uhuru Kenyata nchini Kenya


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kimoon (kulia) na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata (kushoto)

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye amefanya safari nchini Kenya amesisitiza sana juu ya udharura wa kupambana na ugaidi katika mazungumzo yake ya Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo.


Ban Ki-moon amesema kuwa wasiwasi wa mashambulizi ya kigaidi hauishii katika nchi za mashariki na magharibi mwa Afrika, bali dunia nzima inakabiliwa na hatari hiyokubwa tangu Oktoba mwaka 2011 wakati serikali ya Kenya ilipotuma majeshi yake nchini Somalia kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi ya kigaidi ya kundi la al Shabab, watu karibu 300 wameuawa nchini Kenya katika mashambulizi 66 ya kigaidi yaliyokwisha sajiliwa hadi hii leo.
Wiki iliyopita pekee zaidi ya watu 60 waliuawa katika shambulizi lililofanywa na watu wasiojulikana katika eneo la Mpeketoni kwenye Kaunti ya Lamu huko pwani mwa Kenya.
 Licha ya kwamba kundi la al Shabab la Somalia limetangaza kwamba ndilo lililofanya mashambulizi ya Mpeketoni lakini Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anasema mashambulizi hayo yalifanywa na wahalifu wanaodhaniwa kuw na ushirikiano na vyama vya upinzani.
Vyombo vya usalama wa Kenya vimemtia nguvuni Gavana wa Lamu, Issa Timamy kutoka chama cha upinzani cha UDF na washukiwa wengine 13 kwa uchunguzi zaidi unaohusiana na mashambulizi hayo.

No comments:

Post a Comment