Shamba mpunga la Uyole Mbeya |
WAKULIMA
Mkoani Mbeya wameshauriwa
kupanda mbegu zilizothibitishwa na mamlaka ya uthibiti wa mbegu nchini
ili waweze kuepukana na ugonjwa wa zeruzeru kwa zao la mahindi na mazao
mengine.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu
Mratibu wa Afya ya Mimea Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Emmanuel Joo, wakati wa
mahujiano na Mbiu ya Maendeleo mapema
leo ofisini kwake.
Amesema baadhi ya wakulima wamekuwa
wakilima kwa mazoea bila kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo hali
inayopelekea kushuka kwa kiwango cha uzalishaji.
Kaimu huyo ameongeza kuwa mkulima
anatakiwa kusafisha shamba na kuondoa masalia ya mazao ya msimu uliopita ili
aweze kuepukana na ugonjwa huo kwani bado haujapatiwa kiwatilivu chochote cha
kuutibu.
Hata hivyo, ameiomba serikali ifanye
utafiti wa kina kuhusu ugonjwa huo wakati wakulima wanaendelea kuchukua
tahadhari ya kupanda mbegu bora na kusafisha mashamba yao.
No comments:
Post a Comment