SYRIA
imeshindwa kutimiza matakwa ya mwisho yaliyotolewa na jumuiya ya kimataifa
kuitaka iharibu silaha zake za kemikali hivi leo.
Rais
Bashar al Assad alikamilisha zoezi la kutoa silaha zilizotambuliwa rasmi juma
lililopita, hii ikiwa ni miezi kadhaa baada ya siku ya mwisho iliowekwa na
jamii ya kimataifa.
Bado
kuna wasiwasi kwamba huenda Syria bado imehodhi zana zaidi za kinuklya.
Silaha
hizo zitaharibiwa katika meli ya Marekani ya MV cape Ray katika eneo
lisilojulikana ndani ya bahari ya Mediterenean.
Shughuli
hiyo itachukua takriban siku sitini lakini bado kuna wasiwasi kuhusu kuwepo kwa
silaha za kemikali ndani ya Syria.
Mwishoni
mwa juma, usalama zaidi uliwekwa katika bandari ya Gioia Tauro nchini italy.
Vilevile
vizuizi vya ukaguzi vimewekwa katika bandari hiyo.Kati ya tarehe moja na tatu
mwezi July,kilomita moja ya eneo ambalo ndege hazifai kuruka litawekwa.
Makasha
yaliojaa vifaa vya kutengeza silaha hatari duniani ndani ya meli moja ya
Denmark Ark Futura yatafunguliwa na vifaa hivyo kuingizwa katika meli ya MV
Cape Ray.
Lakini
shirika la kukabiliana na silaha za kemikali duniani limekiri kwamba kuna uwezekano
mkubwa kwamba rais Bashar Al Asaad bado anaficha vituo vya siri vya kemikali,na
kuna wasiwasi zaidi kuhusu madai ya utumizi wa gesi ya klorine na wataalam wa
kijeshi wameonya kuwa makundi yenye itikadi kali nchini Syria yanamiliki silaha
za sumu.
No comments:
Post a Comment