Mwanariadha wa Afrika kusin Oscar Pistorius |
MWANARIADHA wa
Afrika Kusini Oscar Pistorius hakuwa na tatizo lolote la kiakili wakati
alipomuua mpenzi wake mwaka jana.
Haya
ni matokeo ya uchunguzi wa kiakili aliofanyiwa Oscar Pistorius huku kesi yae
ikianza kusikilizwa tena nchini Afrika Kusini.
Ripoti
hiyo iliwasilishwa baada ya uchunguzi kufanywa kuhusu hali yake ya kiakili
wakati alipofanya mauaji hayo mwaka jana.
Mawakili
wake walikuwa wamedai kuwa Pistorius aliukuwa anakumbwa na hali ya wasiwasi na
kuzongwa na mawazo wakati wa mauaji ya Reeva Steenkamp.
Mwanariadha
huyo amekana kumuua kwa maksudi mpenzi wake Reeva Steenkamp akisema kuwa
alimpiga risasi kwa bahati mbaya baada ya kupatwa na wasiwasi akidhani jambazi
alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande
wa mashitaka pamoja na utetezi wamekubali matokeo ya uchunguzi huo.
Upande
wa utetezi sasa unasikia ushahidi wake daktari aliyemkata miguu Pistorius,
Gerry Versfeld, anayetoa ushahidi kuhusu athari za Pistorius kukatwa miguu.
Upande
wa utetezi nao unatarajiwa kumaliza ushahidi wake katika siku chache zijazo.
Bi
Steenkamp, alikuwa na umri wa miaka 29, wakati wa mauaji yake Februari mwaka
jana.
No comments:
Post a Comment