Monday, June 23, 2014

CHANZO cha mapigano ya DRC na Rwanda ni kugombea ardhi


Mipaka ya nchi za maziwa makuu

WACHUNGUZI kutoka jumuiya ya mataifa ya eneo la maziwa makuu wamechapisha ripoti kuhusu mapigano ya hivi karibuni yaliyotokea katika eneo la mpaka kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda.


Ripoti hiyo inasema kuwa mapigano hayo yalitokana na mzozo wa ardhi kati ya mataifa hayo mawili katika maeneo ya milima miwili jirani.

Ripoti hiyo inasema kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa upande wake inasema kuwa Rwanda mara kwa mara haiheshimu mpaka ulio kati ya mataifa hayo mawili na wanajeshi wake huvuka mara kwa mara na kuingia katika Taifa lake.

Hata hivyo ripoti hiyo inasema kuwa mapigano ya hivi majuzi yanatokana na kutokuwepo mpaka kamili kati ya mataifa hayo mawili.

Katika mapigano hayo ya hivi karibuni mataifa hayo yalikuwa yakigombania milima miwili ambayo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilidai yote ni yake huku Rwanda ikisema inamiliki mlima mmoja.

No comments:

Post a Comment