![]() |
| Wanajeshi wa Ufaransa nchini Afrika ya kati(CAR) |
HALI ya
mambo ya Jamhuri ya Afrika ya Kati bado ni mbaya licha ya kuweko maelfu ya
wanajeshi wa Ufaransa nchini humo.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le, amesema kuwa hali ya Jamhuri ya
Afrika ya Kati hairidhishi,hivyo juhudi kubwa zinapasa kufanywa ili kutafuta
suluhisho la mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Amesema kuwa viongozi wa kisiasa wa nchi za
Kiafrika wanajukumu la kuchangia jitihada za kutafuta suluhisho la mgogoro wa
Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa amewapongeza pia
wanajeshi 2000 wa nchi yake ambao walitumwa Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu
mwezi Disemba mwaka jana.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa anavipongeza vikosi vya nchi yake vilivyopo Jamhuri ya Afrika ya Kati katika hali ambayo duru za habari za Ufaransa siku kadhaa zilizopita ziliutathmini utendaji wa miezi sita wa vikosi vya Ufaransa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwa ni dhaifu san

No comments:
Post a Comment