Tuesday, June 24, 2014

JUMLA ya miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 1 imezinduliwa na mwenge wilayani Kilombero


Mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala

JUMLA ya miradi 7 yenye thamani ya shilingi bilioni 1,029,561,685imepitiwa na mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2014 katika wilaya ya
Kilombero.


Akisoma risala ya utii kwa Rais,mkuu wa wilaya ya Kilombero HassanMasala alisema kati ya miradi hiyo mradi mmoja umefunguliwa ambao nimaabara ya shule ya sekondari Mlabani iliyopo mjini Ifakara, miradimiwili imezinduliwa ambayo ni nyumba ya mganga Sagamaganga na mashineya kusaga na kukoboa Mang'ula A, na miradi mitatu imewekwa jiwe la
msingi.
  Masala ameitaja miradi iliyowekwa jiwe la msingi ni pamoja na barabaraya Lami ya Uhuru ya mjini Ifakara,mradi wa maji Signal na ofisi yakijiji Mang'ula A huku pia mwenge huo ukipitia na kujionea miradi yavikundi vya wanawake,wanaume,vijana,mradi wa ufugaji nyuki na hifadhiya mazingira na pia kuona shughuli za kupambana na kuzuia rushwa.

Akifafanua gharama za fedha za miradi iliyopitiwa na mbio zamwenge,Masala alisema fedha hizo zimechangwa na wananchi kiasi chashilingi milioni 136.9,serikali kuu kiasi cha shilingi milioni463.8,halmashauri kiasi cha shilingi milioni 5.8 na wahisani shilingimilioni 422.9 na kufanya jumla ya gharama ya shilingi bilioni
1,029,561,685.

No comments:

Post a Comment