![]() |
| Wachezaji waislamu kombe la dunia2014 |
MJUMBE mwandamizi wa Kamati ya Afya ya
Shirikisho la Soka Duniani FIFA amesema kuwa, wachezaji Waislamu watakaofunga
mwezi mtukufu wa Ramadhani, hawataathirika kiafya wakati wa kuendelea michuano
ya kombe la dunia nchini Brazil.
Jiri Dvorak amesema
kuwa, Kamati ya Afya ya Fifa imefanya uchunguzi na utafiti wa kina kuhusiana na
afya za wachezaji katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kufikia natija hii
kwamba, iwapo wachezaji Waislamu watakula vyakula vinavyohitajika,
hawatadhoofika kimwili katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Drovak ameongeza kuwa, kamati hiyo imefanya uchunguzi wa
kutosha, hivyo hakuna ulazima wowote kwa wachezaji kuingiwa na wasiwasi
kutokana na michuano hiyo kuingiliana na mfungo wa mwezi wa Ramadhani.
Wakati huohuo, Michel D'Hooghe Mwenyekiti wa Kamati ya Afya
ya FIFA amesema kuwa, hakutakuwa na tatizo lolote kwani utaratibu utakuwa kama
ule uliofanyika wakati wa michuano ya Olimpiki iliyofanyika 2012 mjini London,
Uingereza. Inatarajiwa kwamba, Waislamu wataanza kufunga mwezi mtukufu wa
Ramadhani kuanzia siku ya Jumamosi au Jumapili ijayo

No comments:
Post a Comment