Monday, June 23, 2014

MWANAMKE aliyehukumiwa kifungo nchini Sudan huenda akaachiwa huru



Bi Meriam Ibrahimu aliyehukumiwa kifungo nchini Sudan

MWANAMKE aliyehukumiwa kifo nchini Sudan Bi Merian Ibrahimu akiwa amejifungua mtoto akiwa kizuizini  huenda akaachiwa huru siku chache zijazo
.

Ripoti zilizotolewa mwishoni mwa wiki  ziliarifu kwamba afisa mmoja wa serikali alithibitisha Meriam Ibrahim, aliyejifungua mtoto akiwa kizuizini ataachiliwa katika siku chache zijazo.

Lakini wizara ya mambo ya nchi hiyo imesema kuwa Bint  Ibrahim anaweza tu kuachiliwa ikiwa kesi yake ya rufaa itafanikiwa.

Bi  Meriam Ibrahim, alilelewa na mama aliyekuwa mkristo , lakini mahakama ilimhukumu kifo ikisema kuwa anapaswa kuwa muisilamu, hiyo ndiyo iliyokuwa dini ya babake.

Alikataa kusilimu na kusema kuwa yeye ni mkristo na hivyo anakabiliwa na hukumu ya kunyongwa kwa kosa la kuasi dini.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Abdullahi al-Azreg, aliwaambia waandishi wa habari kuwa , Bint  Ibahim ataachiliwa huru kwani serikali ya Sudan inawapa watu uhuru wa kuabudu na hivyo iko tayari kumlinda.
Mumewe Meriam Daniel Wami, alisema kuwa taarifa za mkewe kuachiliwa ambazo amezisikia kupitia vyombo vya habari, ni kama uvumi tu.


No comments:

Post a Comment