Monday, June 23, 2014

SERIKALI yagundua muarobaini kwa mawakala wabadhirifu wa pembejeo za kilimo


Dk Mary Mgonja akiwa katika shamba la mtama mkoani Singida

HATIMAE dawa ya kukomesha Mawakala wabadhilifu wa pembejeo nchini imekamilika kwa kutungwa sheria ya pembejeo itakayo komesha kabisha uchakachuaji na wizi kupitia pembejeo nchini


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi msaidizi  kitengo cha usambazaji wa pembejeo za kilimo kutoka wizara ya kilimo na ushirika Kanuti Komba wakati akizindua nembo ya  chama  cha mawakala wa mbegu nchini (TANADA) na kuwasisitiza kuacha tabia hiyo vinginevyo watafilisika na kuishia jela. 

Katika uzinduzi huo uliowakutanisha mawakala hao kupitia wawakilishi na wajumbe toka kanda ya Ziwa,Magharibi, kati,kusini na Kasikazini,Komba alisema serikali imechoshwa na kelele zisizo na tija juu ya hujuma zinazofanywa na mawakala hao kwa wakulima.

Akithibitisha kuwa biashara ya pembejeo 'inalipa'kwa mfanya biashara alionyesha kushangazwa na baadhi yao kuharibu dhana ya serikali kumwezesha mkulima ili azalishe zaidi kwa kuwachakachulia na kuwaibia ili wajinufaishe zaidi.
 
Kwa upande wake wakilishi wa Alliance  for Green Revolutin in Africa (AGRA) ambao ni wafadhili wa mawakala wa pembejeo za kilimo nchini Dk Mary Mgonja alisema shirika hilo limeamua kuwafadhili mawakala hao baada ya wakulima hao kuwa na tatizo la usambazaji wapembejeo vijijini.

Alisema AGRA imejipanga kikamilifu kuhakikisha linafadhili kila kanda kwa lengo la kutoa
elimu ya usambazaji wa pembejeo kwa lengo la kukuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa wakati.

Awali mwenyekiti wataifa TANADA Michael Mahicha na mwenyekiti wa TANADA Mkoa wa Morogoro Amini  Lubegete walimwambia mgeni rasmi kuwa wameanzisha chama hicho kwa lengo la kusaidia serikali inafanikisha malengo yake kupitia kilimo kwa kugawa pembejeo kwa njia sahihi hasa vijiji.
walisema wameamua kufanya hivyo ili iwarahisishia kuwabaini na kuwabana wenye tabia mbaya ya kujinufaisha kwa kutoa huduma duni kwa wakulima ambapo pia wanakusudia kuanzisha chama cha kuweka na kukopa SACCOS ili kuwezeshana kufikia lengo la taifa.

Aidha waliiomba serikali kushirikiana na naokuweka mkakati kuwadhibiti wasambaza pembejeo feki kwa njia mbalimbali ikiwemo ya kushitakiwa na kufutiwe leseni zao maisha.












No comments:

Post a Comment