![]() |
| Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera |
MKUU wa mkoa wa Morogoro Joel
Bendera ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Kilombero kwa hati safi katika
miaka mitatu mfululizo na kuzitaka halmashauri nyingene tano zilizobaki katika
mkoa huo kujifunza wilayani Kilombero
.
Akizungumza kwenye baraza maalumu la madiwani wilayani humo
Bendera alisema kuwa juhudi zinazofanywa na halmashauri hiyo ni hazina tosha ya
maendeleo ya mkoa hivyo halmashauri zilizobaki hazina budi kuiga maramoja
ufanisi wake.
Hata hivyo mkuu huyo alishangazwa na baadhi ya kuendekeza mikopo
hewa,uwasilishaji taarifa zisizo kiwango cha kimataifa,michanganuo isiyoeleweka
kwenye mapato na matumizi na halmashauri kutorejesha asilimia 20 ya mapato
kwenye vijiji.
Kwa upande wake mkaguzi mkazi wa Morogoro Silvester Kibona hoja za
nyuma za halmashauri hiyo zilikuwa 97 lakini hivi sasa zimetekelezwa hoja 90 na
zimebaki 7 na hizo zilizobaki zinahitajika zitoke kabisa.
Awali mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Azimina Mbilinyi alisema mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG alilazimika kutoa hati safi kwenye halamashauri hiyo baada ya kulidhiswa na ubora wa hesabu za kwa mwaka wa fedha 2012/2013

No comments:
Post a Comment