Monday, June 23, 2014

MWENGE wa uhuru kuwasili wilayani Kilosa leo


Mkuu wa wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka akipokea mwenge wa uhuru

MWENGE wa uhuru unatarajiwa kuwasili wilayani kilosa mkoani Morogoro
june 23 mwaka huu ukitokea wilaya kilombero na mapokezi yatafanyika
mapema asubuhi maeneo ya Ruaha Darajani.



Taarifa iliyotolewa na mkuu wa wilaya ya kilosa Elias tarimo june 20
mwaka huu kwenye kikao cha mwenge wilayani kilosa kilichofanyika
kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya kilosa imethibitisha
kukamilika kwa maandalizi yote muhimu na kwamba anaamini mbio za
mwenge kiwilaya zitahitimishwa salama.

Tarimo ameeleza kuwa mwenge wa uhuru wilayani kilosa utakimbizwa
umbali wa km 168 na utapita tarafa mbili kati ya saba kata sita kati
ya 35 na miradi saba ya maendeleo iliyobuniwa na serikali kwa
ushirikiano na wananchi yenye thamani ya shilingi 1,215,162,920
itazinduliwa na mingine kuwekwa mawe ya msingi.

Ameitaja baadhi ya miradi hiyo ni mradi wa kutoa huduma ya maji katika
mji mdogo mikumi,mradi wa msitu wa hifadhi wa kijiji cha Ihombwe,mradi
wa mashine yakukoboa na kusaga nafaka ya vijana nyaranda
mradi wa kituo cha afya ulaya na mradi wa ujenzi wa ofisi ya kijiji na
masjala ya ardhi Msolwa

Aidha Tarimo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuuraki mwenge wa
uhuru kwa maeneo yote ambako mwenge utapita wilaya yakilosa itakabidhi
mwenge kwa ungozi wa mkoa asubuhi ya june 24 na mkuu wa mkoa wa
morogoro Joel Bendera atakabidhi kwa mkoa wa Iringa katika maeneo ya
Ruaha mbuyuni.

No comments:

Post a Comment