Monday, June 23, 2014

WANAWAKE nchini wametakiwa kuifahamu vyema bajeti ya nchi



NAIBUMKURUGENZI wa Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP Lilian Liundi amewataka wanawake nchini kuijua bajeti ya nchi kisera na kisekta kisha kuwa mstari wa mbele kuifuatilia ili iwasaidie kutathimini na mafanikio yake kwao.


Mbali na hilo pia ameishauri jamii kuzielewa vema sera za kisekta nchini ili kuwapa uwezo wa kuhoji baada ya kutambua mafanikio na changamoto zake katika upatikanaji wa maendeleo kupitia bajeti zilizopo.

Akifungua mafunzo wanawake ngazi ya jamii na waandishi wa habari katika ofisi za mtandao huo,Lilian alisema bajeti nyingi hazifikii malengo yake katika utekelezaji kutokana na uelewa mdogo juu ya bajeti hizo sambamba na umuhimu wake katika maisha ya kila siku katika jamii.

Awali mkuu wa Taasisi ya mafunzo katika mtandao huo Ziki Mihyo aliwataka watanzania hususani wanawake kutengeneza mkakati wa ushawishi na utetezi katika masuala ya bajeti katika maeneo walipo ili utekelezwaji wake uende sambamba na matakwa ya sera na mahitaji ya jamii.
.
Jumla ya wanawake,waandishi wa habari 35 kutoka vituo na vyombo mbalimbali vya habari nchini wapo jijini Dar es salaam katika mafunzo ya utambuzi wa bajeti na ushiriki wake katika kujiletea maendeleo ya kiuchumi kwenye jamii na taifa kwa jumla.

No comments:

Post a Comment