![]() |
| Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeresi |
ALIYEKUWA Diwani Mstaafu wa kata ya Mkwatani wilayani
Kilosa Mkoani Morogoro kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Amina Mwarabu
amefariki ghafla nyumbani kwake alfajiri ya june 19 mwaka huu.
Akizungumza
na Mbiu ya Maendeleo mjini Kilosa, mtoto mkubwa wa marehemu,Bwana
Ally Nassoro amesema kuwa mama yake alikuwa na maradhi ya moyo na
kisukari ambayo yalikuwa yakimsumbua kwa muda mrefu na alikuwa anaendelea
kutumia dawa hali inayosadikika kuwa imesababisha kifo hicho.
Aidha
Nassoro ameongeza kwa kusema kuwa marehemu mama yake amefariki akiwa na umri wa
miaka 62 na ameacha jumla ya watoto wane wakiwemo wa kiume watatu na wa kike
mmoja.
Akiongeza
kwa niaba ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilosa katibu Msaidizi Twaribu
Kassimu Kaberege amesema kuwa msiba huo wameupokea kwa masikitiko makubwa kwani
marehemu alikuwa Mwenyekiti mstaafu wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Wilaya
ya Kilosa na pia alikuwa makamu mwenyekiti msaidizi wa Baraza la Wazee Wilaya
ya Kilosa.
Kaberege
amesisitiza kwa kusema kuwa hilo limekuwa pengo kubwa kwa jamii ya Kilosa na
Taifa kwa ujumla kwani marehemu alikuwa mstari wa mbele katika kupigania
maendeleo ya watanzania.

No comments:
Post a Comment