![]() |
| Naibu waziri wa mambo ya ndani Pereira Ame Silima akiongea bungeni mjini Dodoma |
SERIKALI imekiri kuwa baadhi
ya askari polisi na hata wa magereza , Hawana makazi yanayoridhisha hatua
inayosababisha wazazi kukosa faragha wanayohitaji katika jamii.
Naibu
waziri wa mambo ya ndani ya nchi PEREIRA AME SILIMA, amesema hayo jana bungeni
mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalumu, SUZAN LYIMO
kupitia chama cha chadema katika swali lake lililosema askari polisi Nchi nzima
wanashida ya makazi ambayo imesababisha hata faragha ya wazazi kukosekana kwa
kuwa wanashirikiana chumba kimoja na watoto.
Akifafanua
juhudi za serikali za kukabiliana na hali hiyo SILIMA amesema tatizo hilo si la
polisi pekee bali hata askari wa magereza lakini serikali imeanza kujenga
ghorofa sehemu mablimbali Nchini ili familia hizo zipate nafasi zaidi.
Kwa
mujibu wa Silima pia jeshi la polisi limeanziasha shirika litakalokuwa na kazi
maalumu ya kushughulikia makazi ya askari ili kazi hiyo iwe endelevu na
hatimaye changamoto hiyo iishe.
Awali
katika swali la msingi mbunge wa mbogwe Augustino Masele amesema kuna
malalamiko kuwa wakuu wa polisi wa wilaya wamekuwa wakikosa mafuta kwa ajili ya
utendaji kazi wa kila siku ambapo akaitaka serikali itoe ahadi ni lini
itaanza kupeleka fedha hizo za mafuta moja kwa moja kwa wakuu wa polisi badala
ya kupitisha kwa makamanda wa polisi wa Mkoa .

No comments:
Post a Comment