Friday, June 20, 2014

IDADI ya wakimbizi yaongezeka duniani

Wakimbizi nchini Syria

SHIRIKA la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, linasema idadi ya watu waliopoteza makao yao na kufanywa wakimbizi kutokana na vita ilizidi milioni hamsini mwaka jana.
Idadi hii inasemekana kuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu vita vya pili vya dunia.
Vita nchini Syria, ni moja ya sababu kuu ya kuongezeka kwa idadi hiyo ya wakimbizi, lakini pia kuna mizozo mingine katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na nchini Sudan Kusini ambayo imechangia idadi kubwa ya wakimbizi
Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR, linasema kuwa idadi hiyo ni ishara tosha ya athari za kukosa kuzuia mizozo. Pia limesema kuwa mataifa tajiri yanapaswa kufanya juhudi kuhifadhi wakimbizi hao.






No comments:

Post a Comment