Friday, June 20, 2014

RAISI wa Malawi kufunga ndoa mwishoni mwa wiki



Raisi Mteule wa Malawi Prof Peter Mutharika
RAISI mteule wa  wa Malawi  Prof  Peter Mutharika anatarajiwa kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa muda mrefu,mwishoni mwa wiki.,Imeelezwa
Taarifa hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya Rais.
Kwa mujibu wa Taarifa toka Ikulu ya nchi hiyo ni kuwa,: ''Ikulu ya Rais ina furaha kuwajulisheni kuhusu harusi ya kitamaduni itakayofanywa kati ya Rais Arthur Peter Mutharika na mwandani wake wa muda mrefu Madam Gertrude Hendrina Maseko.''
Taarifa hii iliwasilishwa na msemaji wa Rais Chikondi Juma aliyesema kuwa sherehe ya harusi itakuwa ya faragha.
Rais Mutharika aliibuka mshindi katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi jana ambapo mshindani wake mkubwa alikuwa rais aliyeondoka mamlakani Joyce Banda.
Rais Mutharika amewaambia maafisa wa serikali kuhakikisha kuwa hakuna pesa za serikali zitatumiwa katika shughuli hiyo.

Mutharika, mwenye umri wa miaka 74 na ambaye mkewe alifariki , ana watoto watatu, wasichana wawili na mvulana mmoja.

No comments:

Post a Comment