Friday, June 20, 2014

VITAMBULISHO vya wananchi kutolewa septemba mwaka huu

Jaji mstaafu Damiani Lubuva akiongea na waandishi wa habari

MWENYEKITI wa Tume ya uchaguzi (NEC) Jaji mstaafu DAMIANI LBUVA amesema kuwa vitambulisho vya kupiga kura nchini vitatolewa upya kwa wananchi wote ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura.

Ameyasema hayo hivi karibuni wakati akifungua mkutano kati ya tume na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu uboreshwaji wa daftari la wapiga kura.
Jaji LUBUVA ameeleza kuwa mchakato huo wa kutoa vitambulisho upya utakaotekelezwa septemba mwaka huu utagharimu sh bilioni 293 Tofauti na vitambulisho vyaawali vya karatasi vilivyotolewa kwa mara ya kwanza mwaka 2004 kutokana na matumizi ya teknolojia mpya katika uandikishaji.
Ameongeza kuwa katika uboreshaji huo wapiga kura wa zaman kwa maana waliokuwa kwenye daftari la sasa watatakiwa kwenda katika vituo vya kujiandikisha kuchukuliwa taarifa zao hasa alama za vidole picha na saini zao katika mfumo mpya wa BVR na hatimaye kupewa vitambulisho vipya.

Aidha Jaji LUBUVA amesema vitambulisho hivyo vipya vitatolewa papo hapo uandikishaji ukikamilika na vitakuwa vya plastiki ngumu na namba ya mpiga kura.



No comments:

Post a Comment