![]() |
| Watoto nchini jamhuri ya Afrika ya kati(CAR) |
MASHIRIKA mawaili ya Umoja wa Mataifa yamesema kuwa, karibu watoto milioni
30 wa shule za msingi hawaendi shule barani Afrika kutokana na umasikini na migogoro
.Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) na
Shirika la Umoja wa Mtaifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yamesema
kuwa, watoto milioni 19 hawaendi shule huko magharibi na katikati mwa Afrika na
wengine milioni 10 hawahudhurii shuleni katika maeneo ya kusini na mashariki
mwa bara hilo.
Ripoti za mashiria hayo zimeeleza kuwa, matatizo ya fedha
yanayoisumbua dunia nzima na machafuko katika bara la Afrika pia vimekwamisha
jitihada za kuwarejesha watoto shuleni.
Yumiko Yokozeki, mshauri wa elimu wa UNICEF amesema, shule nyingi
zimefungwa katika nchi zenye machafuko za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nigeria na
Mali.

No comments:
Post a Comment